Loading...
Loading...

Professor Jay Ft Diamond - Kipi Sijasikia ( Audio With Lyrics )
play in 3gp Mp4 Flv Webm Mp3 available in 240p, 360p, 4800p, 720p, 1080p video formats

 • Uploaded on 23 Jun 2014

  Buy it from iTunes: https://geo.itunes.apple.co...
  Niliacha kazi nifanye muziki wakatabiri nitalost, Wengine wakanishawishi tuloge kuondoa mikosi, Nakomaa na muziki ingawa jua la utosi, Naamini wote tunapita na kamwe maiti haijioshi Jina langu lishatumika sana kutajirisha watu, Nyota ndogo alishasema kuna Watu na viatu, Bunduki haiui watu ila watu ndio wanaua watu, Dunia kama jalala tazama kwa Jicho la Tatu,
  Ni saa mbaya watu wanahusda na roho mbaya , Tunawaita watakatifu kumbe ndio mavimpire, Yalisemwa mengi demu wangu alivyotoroka, Ni Fundisho tosha na changamoto kwa Mwanachoka Nimepita Mengi mitihani ya kila Namna,
  Ndio maana mi sishangai wakiniita mbeba Lawama,
  Washkaji wengine fake kwenye deal hawakujui Wanadhani kila jogoo akiwika ni Asubuhi,
  Riziki hamuwezi iziba labda mtaichelewesha tuu,
  Mnakesha mnishushe Mwenyezi ananipaisha,
  Kote mlikobana kidume ndio Natusua,
  Mnanijua,Nakamua, Roho za wanga zinaungua
  PLATINUM!!!

  CHORUS;
  Unaehukumu ni wewe Mwenyezi Mungu naomba unilindeee..
  Kwenye hii vita milele Basi nishike mkono nishindeee..
  Unaehukumu ni wewe Mwenyezi Mungu naomba unilindeee..
  Kwenye hii vita milele Mwanachoka daima Nishindeee..

  VERSE 2
  Walishazusha nimekufa, Eti nimepata ajali,
  Washindwe na walegee Mwenyezi niepushie mbali
  Wakasema nina Ukimwi kwa kuwa nilikonda ghafla,
  Wanataka kunizika mzima Kabla sijafa,
  Waliosema nina Ngoma wengine tushawafukia, Wanaoomba nife leo naamini Watatangulia,
  MAMA Pumzika Pema..Daima tunakulilia,
  Na bado wanachonga sana but MAN the KING is here!!
  Daima mtaji wangu ni nguvu zangu mwenyewe, Simwamini mtu kamwe najiamini mi mwenyewe, Hata nikinywa maji wanadai nakunywa pombe, Mi sijali, I KNOCK THEM HARD Mwanalizombe! Bado tu napambana kibarua kisiote nyasi,
  Daima sitawadhuru wale wote walioniasi,
  Nikikaa kimya msidhani Sijasikia,
  Sio Bahati sio Ngekewa ni sauti Iliyobarikiwa HOLLA!!!

  CHORUS;

  Verse 3
  Mungu walaze pema Waliosemwa wakajiua,
  Ingawa wote tunapita naamini Maisha ni hatua, Maneno ya watu Sumu, Yanaponya na Yanaua, Please nipe ujasiri mpaka siku Ukinichukua,
  Wape nguvu wale wote waliokata tamaa, Maneno yanaleta hila na Mzozo kwenye mitaa, Wanahesabu mabaya tuu na mema hawayaoni, Wanakuchekea Machoni, Wanakuroga Moyoni,
  Wanacheka chinichini wakati una Msiba,
  Wa kwanza kukutangaza kwa watu ukiwa na Shida!!
  Wanatamani wapangue kila mola alichopanga, Wanatangaza Amani huku wameficha MAPANGA

  CHORUS;

  Channel ProfessorJay

TAGS:

Loading...

You Might Also Like

Recent Movies

Youtube Hatena . Webry . bd . Tripod . Addto . So-net . Gamer . Google+ . Facebook -- Hson-- ucz-- gd-- one-- goggle-- zestr-- jobstu-- multiple-- colt-- sandy-- exp-- gou-- myapp-- nap-- msu